Kama una picha au video katika Albamu za Picasa kwenye Wavuti, njia rahisi ya kuzifikia, kuzirekebisha na kuzishiriki ni kuingia katika akaunti ya Picha kwenye Google. Utapata picha na video zako hapo.
Kwa wale ambao tayari wameipakua, itaendelea kufanya kazi kama kawaida. Lakini hatutaiboresha na haitapokea masasisho mengine.
Ukichagua kwenda katika huduma ya Picha kwenye Google, unaweza kuendelea kupakia picha na video ukitumia kipakiaji cha eneo-kazi katika photos.google.com/apps.